Mark 6:53-56

53 aWalipokwisha kuvuka, wakafika nchi ya Genesareti, wakatia nanga. 54Mara waliposhuka kutoka mashua yao, watu wakamtambua Isa. 55Wakaenda katika vijiji vyote upesi, wakawabeba wagonjwa kwenye mikeka ili kuwapeleka mahali popote waliposikia kuwa Isa yupo. 56 bKila mahali Isa alipokwenda, iwe vijijini, mijini au mashambani, watu waliwaweka wagonjwa wao masokoni. Wakamwomba awaruhusu hao wagonjwa waguse japo upindo wa vazi lake. Nao wote waliomgusa waliponywa.
Copyright information for SwhKC